BENKI ya Exim Tanzania yatangaza uzinduzi wa chumba maalum kipya chenye kiwango cha juu cha kufuatilia kamera za ulinzi zilizopo katika matawi yote ya benki hiyo nchi nzima. 

Uzinduzi wa chumba hiki kipya kinaonyesha juhudi za benki hiyo katika matumizi ya teknolojia na uvumbuzi ili kuhakikisha kuwa benki yenye mazingira ya usalama sio tu kwa wateja bali kwa wafanyakazi pia. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha kuzuia hatari na uhakiki (Risk& Compliance) David Lusala amesema kuwa “Benki ya Exim imejikita katika kutengeneza mazingira ya usalama kwa wateja wake. Tuna timu nzima iliyopata mafunzo husika katika masuala ya usalama ambao wana jukumu la kuhakikisha shughuli zote zinarekodiwa na kusimamiwa ipasavyo. Kitu chochote kitakachoonekana kuwa hakiko sawa kitagundulika kwa haraka na hatua za haraka kuweza kuchukuliwa. Tungependa wateja wajue kuwa tutakuwa na taarifa za wakati pale ambapo kutatokea kitu chochote kibaya.” 

Katika kitengo cha kutoa taarifa kinachojulikana kama ‘whistle blow’ Lusala alitoa wito kwa wadau kufanya kazi kwa karibu na benki katika kutoa taarifa ya mambo yoyote ya hujuma. Hii inaenda sambamba na kampeni ya kuzuia udanganyifu iliyozinduliwa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa maadhimisho ya miaka 19 ya benki. 

Kampeni ya kuzuia hujuma inalenga kutengeneza mazingira ya kutokuwa na udanganyifu katika sekta ya benki kwa kushirikisha umma kuweza kutoa taarifa za shughuli zozote za kihujuma katika benki. Umma unahimizwa kutoa taarifa hizo kupitia barua pepe eximbank@tip-offs.com au kupiga simu ya bure kupitia namba 0800 11 0050.

“Tunatambua umuhimu wa mchango wa wafanyakazi na wateja wa benki yetu, kampeni hii inalenga kujenga mazingira ya uwazi na usalama ili kuwapa fursa wadau wetu kuweza kutoa taarifa hizi bila woga,” ameongeza Lusala. 

Benki ya Exim Tanzania ni moja ya benki tano bora nchini, benki hii inaendelea kujivunia kuwa mwanzilishi katika uvumbuzi na teknolojia. Benki ya Exim Tanzania inahamasisha na kutumia teknolojia kuhakikisha ukuaji wa haraka na kuridhisha wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...