KAMPUNI ya TICTS inayojishughulisha na kazi ya uendeshaji wa huduma za bandari, Dar es salaam imeendelea na kampeni ya yake ya "Go GREEN" kwa kupanda miti katika eneo la Shule ya Sekondari Mivinjeni, Wilayani Temeke.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini hapa, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa alisema ili Tanzania ifikie lengo la kuwa na uchumi wa kati kufikia mwaka 2015, suala la upandaji miti ni lazima kufanyika ili kuenda sambamba mkakati huo.

"Tukiwa na miti michache au miti iliyotoweka, tutaangamia kama taifa na ikiwa tutakuwa na miti mingi, hapo hatuna cha kupoteza, ila tukiruhusu ukataji miti uendelee katika nchi yetu bila kupanda mingine, tutaishia kuwa ombaomba kama si kufa kwa njaa" alisema Talawa.

Pia alitoa wito kwa makampuni mengine yanayofanya biashara hapa nchini, kuisaidia Serikali kuhamasisha masuala yenye manufaa kwa taifa kama hilo la kupanda miti.
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa akishiriki kupanda Mti katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, kupitia Kampeni yao ya "Go GREEN" yenye kuhamasisha jamii umuhimu wa kupanda miti. 
 Meneja wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari wa Kampuni ya TICTS, Hassan Mageta (kati) akimwagilia maji mti wake muda mfupi baada ya kuupanda katika eneo la Shule ya Sekondari Kurasini, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
 Meneja wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya TICTS, Caroline Owenya (kushoto) akishirikiana kupanda mti na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kurasini, Mwl. Marcelino Fussi (katikati) pamoja na mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2016.
Wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS wakipanda miti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...