Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) wakishuhudia. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akipiga makofi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 


Awali akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alisema uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G unaifanya TTCL kuwa Kampuni ya kwanza nchini na eneo lote la Afrika Mashariki kutoa huduma yenye kiwango cha juu kabisa cha kasi na ubora katika huduma za Intaneti. 

Alisema TTCL inaendelea kutekeleza mpango wa mageuzi ya kibiashara ambapo hatua mbali mbali zinachukuliwa katika kuboresha huduma zake. Hatua zinazochukuliwa zinalenga katika kuirejesha Kampuni katika hadhi yake ya kuwa Mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini, kiungo muhimu cha kufanikisha shughuli za ukuaji wa sekta nyingine na mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katikauzinduzi huo alisema, Serikali imepokea taarifa ya uzinduzi wa 4.5G kwa furaha kubwa na kuamini kuwa sasa, TTCL ambayo ni mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini inafanya kile ambacho Taifa zima lilitegemea kupata kutoka kwa Kampuni hii.

 "...Naipongeza Menejimenti na Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa juhudi kubwa za kuleta mabadiliko ya utendaji na uwajibikaji, ambao ni utekelezaji wa mwongozo wa Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais mpendwa Mhe Dkt John Pombe Magufuli," alisema Profesa Faustine Kamuzora.  


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...