Na Mary Margwe, Simanjiro

Imeelezwa kuwa baada ya kumaliza zoezi la kitaifa la ukamilishaji wa madawati kwa asilimia 100% katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara, sasa yageukia upande wa pili wa ujenzi wa madarasa,ambapo imelengwa zaidi kwa Shule za msingi ambapo ndio kwenye uhitaji zaidi.

Akiongea juzi katika mkutano wa baraza la Madiwani, kilichoketi chini ya makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Albert Msole, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Yefred Myenzi, Karibu tawala wa wilaya hiyo Zuwena Omary, alisema baada ya kuhitimisha suala la madawati sasa yageukia ujenzi wa madarasa.
Omary alisema wamefanya zoezi la uhakiki , na katika uhakiki huo wamegundua kuwa madarasa bado hayatoshi , kwa sababu katika uhakiki wao wamekuta chumba kimoja cha darasa linatumika kwa wanafunzi wa madarasa matatu yaani darasa la kwanza, na pili na tatu,ambapo hali imekua Mbaya zaidi kwa upande wa Shule za msingi.

Aidha alisema hali hiyo ni Mbaya katika kumjengea uelewa mtoto anayetakiwa kujengwa kitaaluma,hivyo ni vema hatua za haraka zinahitajika kukamilisha suala la madarasa kama lilivyofanikiwa zoezi la madawati, na hilo nalo likamilike kwa nijia hiyo hiyo.

"Ufaulu wa mtoto ni msingi gani tumemuwekea huyu mtoto,sio sisi kama wazazi tubaki kuhoji kufeli kwa watoto wakati wote,tujiulize na hili, kwani kufaulu ni pamoja na mazingira ya kujifunzia na kujisomea,baada ya kukamilisha hili sasa tuendelee kuhoji mengine mengi tu katika kuleta ufanisi katika kumjengea msingi bora" alisema karibu tawala huyo.

"Kwa hiyo wakati huutumemaliza utekelezaji wa madawati ambalo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, tena napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wilaya ya Simanjiro kiujumla kwa ambavyo tumefanikiwa, sasa twendeni tuhamie kwenye madarasa, haiwezekani na haikubaliki watoto wetu tukiendelea kuwaona wamekalia madawati mazuri, huku wakiwa wamerundikana madarasa matatu kwa moja (yaani three in one) alisema Omary.

Aidha alifafanua na kusema kuuwa katika suala hilo la madarasa hata waheshimiwa madiwani ni mashahidi katika kata wanazotoka wanajua dhahili kuwa hali ikoje, kwani ni mbaya hususani kwenye Shule za msingi,hivyo ni jukumu la Kila mmoja kuhakikisha anatoka kwenye baraza hilo akiwa na wazo jipya la ujenzi wa madarasa ambao ni wa lazima na si wa hiari.

Kufuatia hilo katibu tawala huyo alisema ni vema sasa uongozi wa wilaya ukajipanga wote kwa pamoja ,hukakikisha ni kwa namna gani zoezi hilo linakamilika ama kutekelezeka mara baada ya kujua ni madarasa mangapi yanahitajika,namna ya kupatikana kwake na kwa utaratibu gani.

"Mh.makamu mwenyekiti, kwa hiyo sisi tunasema wilaya yetu tujiunge wote kwa pamoja na tujikite zaidi kwenye ujenzi huu wa madarasa,hivyo tujiandae na sisi huku kama viongozi tunaweka mpango ambayo tutakubalina wote kwa pamoja kuwa nini kifanyike,tunahitaji madarasa mangapi na kupatikana kwake na kwa utaratibu gani na kwa muda gani" alisema karibu tawala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...