Na: Frank Shija, MAELEZO. 

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) takiwa kuhakikisha Chuo hicho kinaendelea kuwa kiongozi miongoni mwa Vyuo Vikuu nchini. 

Ushauri huo umetolewa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akifungua maadhimisho ya miaka 55 ya chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. 

“Hiki ndicho Chuo kiongozi kati ya Vyuo Vikuu vyote hapa nchini, mnatakiwa kuhakikisha kinaendelea kuwa kiongozi huku Vyuo vingine vikifuatia”. Alisema Dkt. Kikwete 

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Lwekaza Mukandara amesema kuwa pamoja na changamoto zinazo kikabili chuo hicho wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kusaidia katika kuleta maendeleo ya chuo hicho. 

Alisema kuwa baadhi ya changamoto zimetatuliwa kwa pamoja kati ya Serikali na wahisani ambapo alisema kuwa ujenzi wa kumbi mpya za mihadhara, Maabara za Kisasa na jengo la malazi,pamoja na ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea katika Kampasi ya Julius K. Nyerere ambayo itakuwa na uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 4000 mara itakapo kamilika. 

Akiwasilisha mada juu ya “hali ya Taaluma Barani Afrika katika Muktadha wa Kimataifa” Mhadhiri wa Heshima kutoka nchini Nigeria, Profesa Tade Aina amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja kati ya Vyuo Vikuu mahiri barani Afrika ambapo kimetoa mchango mkubwa kwa ukombozi wa nchi nyingi za bara hili. 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na washiriki wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam. 
Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika muktadha wa Kimataifa wakati wa kongamano la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki wa kongamano maalum la kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria wakati akielezea hali ya vyuo vikuu vya Afrika katika muktadha wa Kimataifa mapema hii leo Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam. 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) wakati wa kongamano la  kuazimisha miaka 55 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema hii leo Chuoni hapo, katikati ni Mhadhiri wa Heshima Prof. Tade Aina toka nchini Nigeria. 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wakuu wa Vitivo wa Chuo hicho wakati wa kongamano la kusherehekea kutimiza miaka 55 toka kuanzishwa kwa chuo hicho. 

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...