Na Yusuph Kileo
Takwimu za uhalifu mtandao zimeendelea kukua huku wana usalama mtandao
wakiendelea kutafuta suluhu ya kudumu dhidi ya uhalifu mtandao maeneo mengi
duniani. Hivi sasa tumefikia wakati wa kila tunavyotumia ku unganishwa kwenye
mtandao (Internet of Things – IoT) ambapo Televisheni, Friji , Majiko, Magari
na kadhalika vimekua vikiunganishwa mtandaoni ili kurahisisha maisha ya
watumiaji.
Hali hii imepelekea wimbi kubwa la uhalifu mtandao kuendelea kukua na
imetabiriwa kadri muda unavyoendelea tishio la uhalifu mtandao litakua kubwa
zaidi – Kuliangalia hili Mkutano wa wana TEHAMA wa Nchi za Afrika (AfICTA) wa
mwaka huu 2016 ambao uliofanyika jijini Windhoek Nchini Namibia ulipata
kujadili mengi kuhusiana na hili ambapo pande mbili za faida na changamoto
ziliangaziwa kwa karibu.
Binafsi, Nilipata kushiriki kuongoza mijadala miwili ambapo tuliangazia
changamoto za ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na wimbi wa vitu vingi
kuendelea kuunganishwa mtandaoni na pia kujadili mapendekezo ya mambo ya msingi
ya kuzingatia ili kubaki salama pamoja na mambo ya msingi kwa wadhibiti wa
uhalifu mtandao wanayopaswa kuzingatia ili kuweza kudhibiti hali hii. Kusoma zaidi BOFYA HAPA.
Usiku wa Jana jijini #Windhoek, Namibia, Mdau mkuu wa Usalama wa Mtandao wa Tanzania Yusuph Kileo amepokea Tunzo yake ya Kwanza ya kimataifa Kubwa katika kutambua mchango wake mkubwa Barani katika swala la Usalama mtandao! Yusupha hakika amemefurahi sana! Kwani jina lake litaingia katika majina yanayotegemewa kujadiliwa ili kuingia katika bodi ya wana TEHAMA wa Nchi za Afrika! Hatua muhimu kwake na Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...