Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe  na Mkurugnzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wamepiga marufuku ufugaji holela. Tamko hilo limetolewa baada ya uongozi wa kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku Ndani kuomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kuwasaidia kuondoa wafugaji waliovamia katika kijiji chao na kuharibu mazao ya kilimo ya wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya aliwaeleza wananchi kuwa kila sehemu kuna taratibu na sheria zake namna ya kuishi. “ni marufuku kuchunga mifugo kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu ya Serikali au ya Kijiji kwa maana  ni kosa akipatikana mtu wa namna hiyo kamateni peleka polisi na mimi nifahamu”alisema, na pia ni marufuku kuchukua mifugo kwenda kuchunga kwenye shamba  la mwenzako kuwepo na  mazao au  hakuna ni kosa kamateni mtu wa namna hiyo  peleka polisi, hata kama mwenye shamba amekwisha vuna isipokuwa kwa idhini ya mwenye shamba pekeyake.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni aliwaeleza wananchi  kwamba ulinzi wa mali za Chogo  ni wanachogo wenyewe, na mgogoro wa wakulima na wafugaji ni wetu sote, Aliwaeleza kwamba walishindwa kuchukua tahadhari mapema pindi wafugaji hao walipoingia miezi mine iliyopita kwa sababu eneo lao lina mpango bora wa matumizi ya ardhi. 

Aidha aliwaeleza wananchi kuwa, amewataka  Watendaji wa Kata na Vijiji kuleta orodha ya mifugo iliyopo kwenye maeneo yao na waeleze uwezo wa ardhi iliyopo kuweza kuhimili idadi ya mifugo iliyopo kwa mujibu wa mpango wa ardhi uliowekwa katika maeneo yao ili kugungua  kama kunamifugo imezidi au haijazidi, “Tarehe 29/10/2016 nitapata orodha ya Halmashauri nzima kwa kata 21 na  Vijiji 91” alisema. 
Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wannchi wa kijiji cha  Chogo  wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akifuatiwa na Mh.Abdalla Pendeza Diwani wa Kata ya Kabuku Ndani na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha chogo. 
 Mkuu wa Wilaya ,Mukurugenzi Mtendaji na viongozi wengine kutoka Halmashauri wakitazama moja ya eneo laKitalu cha kuoteshea miti ya malimao mkulima baada ya kupitia shamba na kuona uharibifu uliofanyika.

baadhi ya wananchi kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku ndani.   
 mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya handeni akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chogo kata ya Kabuku Ndani.
  Mmoja kati ya wafugaji waliopo katika kijiji cha ChogoBw. Masanja akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na  wananchi wote kwa ujumla.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...