Vijana wasomi 53  wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya. 
Vijana hao ni wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini  na nje ya nchi ambao wamejitolea kufnya kazi hiyo nzito bila malipo.
Vijana hao, ambao wameungana katika  grupu la Whatsapp la WAZALENDO,  leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga (wa pili kulia). 
Vijana hao, 14 wakiwa wanawake na 39 wanaume, walikubaliana kupiga kambi shuleni hapo toka Septemba 27, 2016  na kufanya kazi hiyo ya kujitolea na bila malipo kwa moyo mmoja na kufanikiwa kufyatua matofali hayo. Kambi hiyo inatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi Oktoba 29, 2016 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako.
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akipungia pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. I'm proud of you all, ninyi ni wazalendo wa kweli.
    Badala ya kukaa na kusubiria pres. Magufuli ataifanyia nini Tanzania, nyie mlijiuliza mtaifanyia nini nchi yetu. Magroup mengine ya whatsapp igeni mfano huu na kuwa productive badala kupiga siasa maandazi na kulaumu serikali kwa kila kitu. Bravoo

    ReplyDelete
  2. Safi sana bwana michuzi. Hiyo shule niliitembelea mara 2 kati ya 2004 na 2006 kwaajili ya utafiti wa ELIMU NA MAZINGIRA kwa mtoto wa kike. Hali ya shule hiyo ilikuwa mbaya sana na walimu hawakuwa na nyumba. Wazalendo hawa ni Nyerere type. I big up them.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...