Vijana wakiwa katika kikao kidogo cha kuhitimisha kazi
  Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) akisema machache. Yeye alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
 Baada ya kazi nzito Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akijiunga kupata msosi na  vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Vijana hao wasomi 53 wakipata msosi baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Uzalendo mbele - Hadi raha.
    Tunawashukuru sana hawa vijana kwa kujitolea na kuonyesha mfano mzuiri.
    Tukipata vijana kama hawa kila wilaya, Tanzania itakua katika hatua nyingine kimaendeleo miaka mitano mpaka kumi ijayo.

    ReplyDelete
  2. Kwakweli tumethubutu Na tumeweza, njooni tuijenge Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...