Nteghenjwa Hosseah – Arusha 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amechangia mabati 136, mifuko ya Saruji 30 pamoja na Fedha taslimu Tsh 500,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa mabweni mawili yaliyoungua moto hivi karibuni katika Shule ya Sekondari Longido.

Rc Gambo ametoa msaada huo wakati wa ziara yake ya Kikazi wilayani hapo ambapo alitembelea Shule hiyo na kukuta wanafunzi wakilala madarasani tangu Mabweni hayo yalipoungua na uongozi wa Shule hiyo kuamua kutumia madarasa hayo katika kipindi hiki cha mpito wakati wakiwa wanaendela na ujenzi wa mabweni hayo ambayo ujenzi wake unagharimu zaidi ya Tsh Mil 45.

Akisaoma taarifa ya ujenzi wa mabweni hayo Afisa Elimu Sekondari Bw.Gerson Mtera alisema endapo wangetumia Mkandarasi ujenzi huo ungegharimu zaidi ya Ths Mil 75 lakin kwa kuwa wanajenga kwa kutumia mafunzi wa jamii pamoja na wataalamu wa Halmashauri mabweni hayo yatagharimu Tsh Mil 45 tu.

Nimeona jitihada za uongozi wa Wilaya pamoja Shule katika kukabiliana na changamoto hii na jitihada zenu hakika sio za kupuuzia na mimi kama Kiongozi wa Mkoa nawiwa kuchangia kazi hii ili iweze kukamilika haraka na wanafunzi warudi katika malazi yaliyo bora na madarasa hayo yaweze kutumika kwa shughuli stahiki alisema Gambo.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa alikutana na walimu pamoja na wafanyakazi wasio Walimu kusikiliza malalamiko na kubaini baadhi wa walimu kutolipwa malimbikizo ya Fedha za Likizo pamoja na watumishi kuajiwa kwa zaidi ya miaka kumi pasipo kuwa na mkataba wala barua ya ajira kutoka kwa Mwajiri wake.

Akiongea katika Kikao hicho Mhe. Gambo alisemani ni muhimu kwa kila Halmashauri kuwajali watumishi wake haswa walimu na wafanyakazi wa kada za chini ili kuwaongezea ari ya kufanya kazi na kuwatia moyo waweze kutumikia Taifa hili kwa uzalendo sio kila siku mnatoa vipaumbele kwa watumishi wa Kada za juu kufanya hivi mnasababisha matabaka yasiyo ya lazima katika utendaji kazi wenu wa kila siku.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo aliahidi mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia ipasavyo wote wanaohusika na ujenzi wa mabweni ya Sekondari ya Longido ili kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa na kumhakikishia kwamba mpaka mitihani ya Kidato cha nne itkapoanza wanafunzi hao watakua wameshahamia kwenye Mabweni hayo na madarasa hayo yatatumika kwa ajili ya kazi hiyo na baadae wanafunzi wataendelea kuyatumia katika masomo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo(kwanza kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido Mhe. Esupat Mulupa wakielekea kukagua ujenzi wa mabweni katika Shule ya Sekondari Longido . 
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Longido Ndg. Gerson Mtera(mbele) akisoma taarifa ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Longido wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wilayani hapo. 
Ujenzi unaendelea katika mabweni ya Shule ya Sekondari Longido na hivi ndivyo yanavyoonekana kwa sasa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...