Na George Binagi-GB Pazzo
Wadau wa elimu mkoani Mwanza wametakiwa kushirikiana na serikali katika kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za waalimu katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza.

Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Florence Sam, ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta pamoja na printa, vilivyotolewa na wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 1993.

Mwalimu Sam amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1,800 huku vyumba vilivyopo vikiwa ni 18 hali inayosababisha kuwa na upungufu wa vyumba 32 ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa wadau mbalimbali kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo, Mwalimu Benadetha Athanasi, amesema wanafunzi hao wameamua kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za shule hiyo ili kutoa mwamko kwa wadau wengine kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu nchini.

Vifaa vilivyotolewa na wanafunzi hao ni pamoja  na vifaa vya michezo kwa wanafunzi,kompyuta pamoja na printa ambavyo vimegharimu Zaidi ya shilingi Milioni Mbili.

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa Mtendaji wa Kata ya Muhandu ilipo shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

Mbali na vifaa hivyo, pia wanafunzi hao ambao miongoni mwao ni wafanyabiashara na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, wametoa vifaa vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo mipira na jezi, pamoja na zawadi mbalimbali kwa ikiwemo kompyuka kwa baadhi ya waliokuwa waalimu wao kipindi hicho.
Na BMG

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakiwakabidhi baadhi ya waalimu pamoja na kamati ya shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakikabidhi vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...