Makamu mwenyekiti wa ccm Tanzania Bara Mzee
Philip Mangula akitembelea kambi ya Vijana 53 wazalendo Wasomi wetu kutoka vyuo
vikuu vya nje na ndani ya nchi walioungana kwa pamoja kufyatua matofali 45,000
kwa ajili kujenga mabweni 5 pamoja na nyumba 5 za walimu katika shule ya
sekondari Nasibugani wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mh Filberto Sanga alichukua hatua
ya kuandaa kambi hii ya wazalendo kusaidia adha waliyokuwa wakipata wanafunzi
wa shule ya Nasibugani gani ikiwemo kukosa mahala pa malazi huku baadhi yao
kidato cha tano na sita wakilala katika chumba cha maabara.
Ripoti iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wazalendo Bw Daniel
Sarungi inaelezea maisha ndani ya kambi na shughuli walizofanya ikiwemo
Kufyatua matofali, Kusomba Mchanga, Kujipikia chakula, Kufundisha wanafunzi wa kidato cha V na VI, Kutoa huduma ya afya kwa wanakambi na wanafunzi, Mijadala ya maendeo na utawala bora pamoja na Kuhamasisha wanafunzi kujiunga na vilabu vya kupinga
rushwa.
Report hiyo ya wazalendo pia imeomba serikali kama ikiona
inafaa wale wote wanaopenda kufanya kazi serikalini waanze kwa kujitolea miezi
6 au mwaka mmoja ndipo waajiriwe kufuatana na taaluma zao.
Kambi inaongozwa na mwenyekiti wa kambi Mwita Nyarukururu,
Makamu Mwenyekiti ambae ni Helen Madole pamoja na Katibu Mkuu wa wazalendo
Daniel Sarungi.
Mlezi wa kambi ya wazalendo ni kamati ya ulinzi na usalama
wilaya ikiongozwa na Mh DC Filberto Sanga.
Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara mzee Philip Mangula katika picha ya pamoja na kambi la wazalendo wasomi |
Kambi ya wazalendo ilianza tarehe 28/09/2016 na mpaka sasa zaidi ya matofali 38,235 yako tayari na yamebaki matofali 6,765 tu. |
Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara mzee Philip Mangula akichakarika na Wazalendo wasomi
Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara mzee Philip Mangula akiendelea kufanya kazi na Wazalendo wasomi
Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara mzee Philip Mangula akiongea na Wazalendo wasomi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...