Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa majadiliano ya amani na ulinzi kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) unaofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo unarajia kujadili kuhusu masuala yafuatayo; Aina za chaguzi na jinsi zinavyosimamiwa miongoni mwa nchi wanachama, Vijana wa Afrika wanaokimbilia Ulaya kutafuta maisha, tishio la amani ya Kanda na Dunia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (katikati) akifuatilia Mkutano. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (kushoto)
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano na Watendaji wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka SADC na EU.
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...