WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa nchini Tanzania Mhe. Charles Mwijage leo amezindua rasmi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Maisha Plus. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo Mhe. Mwijage alisema kitendo cha washiriki hao 16 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kuweza kubuni mashine ni sawa na kufaulu mitihani mikubwa ya kimaisha. Alisema mashine hiyo ni mkombozi kwa watu wote wa Afrika Mashariki kwa sababu inaweza kusaga bila kutumia umeme lakini pia inamuwezesha mtu kufanya mazoezi. “Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage. Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki. 
Grace PEMBA kutoka Mtwara aula Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane. "Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho." 

Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi. Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter. Maisha Plus inaratibiwa na kampuni ya DMB na vipindi kutengenezwa na kampuni za True Vision Productions, KP Media na Pumzika Communications. 

#VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...