TIMU ya soka ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na kufikisha jumla ya alama 24 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Yanga walioanza kuona goli la JKT Ruvu dakika ya sita ya mchezo kupitia kwa Obrey Chirwa lakini umakini mbovu wa safu ya washambualiaji ulifanya wakose magoli mengi na mpaka kumalizika kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga walitoka mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulisakama lango la JKT Ruvu na katika dakika ya 63 Amisi Tambwe aliyeingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliiandikia Yanga goli la pili na dakika ya 83 Simon Msuva kwa kutumia udhaifu wa golikipa Said Kipao aliyekuwa mwiba kwa safu ya ushambuliaji wa Yanga akaweka kimiani goli la tatu.

Safu ya ushambuliaji ya JKT Ruvu wanashindwa kuwa makini ambapo wanashindwa kufanya mashambulizi ya uhakika na mabeki wa Yanga kuweza kusahihisha makosa yao.

Dakika ya 90, Amisi Tambwe anaiandikia Yanga goli la nne na kupeleka kilio zaidi kwa JKT Ruvu na mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga wanatoka mbele kwa goli 4-0.

Yanga imecheza leo chini ya Kocha Juma Mwambusi baada ya Aliyekuwa kocha mkuu Hans Van De Pluijm kujiuzulu jana jioni.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia mara baada ya kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amisi Tambwe akiachia mkwaju mkali uliotinga moja kwa moja wavuni na kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0.
Mchezaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwania Mpira na Beki wa Timu ya JKT Ruvu, Nurdin Mohamed katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 4-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. KUTAFUTA FURAHA MAISHANI NI KAMA KUMTAFUTA PAKA MWEUSI KATIKA CHUMBA CHENYE GIZA, YANGA MNATAKA FURAHA GANI ZAIDI YA HII, MNAMFUKUZA KOCHA WENU NA MKIJUWA KUWA WACHEZAJI WENU WAMEKAA PAMOJA MUDA MREFU NA MWALIMU WAO HUYO, LEO MNAFANYA KITU KIBAYA SANA, USHAURI WANGU MPENI HIYO KAZI YAKE, MTAANZA KUFUGWA HAPA BURE.

    DR, JAMESSY

    ReplyDelete
  2. naona Yanga wamebadilisha njano yao kimyakimya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...