Golikipa wa Mbao FC, Emanuel Mseja akiruka kudaka mpira bila mafanikio uliokwenda moja kwa moja wavuni baada ya kurushwa na Mchezaji wa Yanga, Mbuyi Twite na kuiandikia timu yake bao la pili katika Mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda goli 3-0.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mbao Fc ya mkoani Mwanza na kufikisha alama 27 nyuma ya alama tano kwa mahasimu wao wa jadi Simba.

Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu sana kwa Yanga hasa baada ya Mbao kuonekana wako makini katika kuhakikisha hawaruhusu goli la mapema na mpaka zinafikia dakika 45 za kipindi cha kwanza timu hizo zilienda mapumziko 0-0.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa Yanga kutafuta goli la dakika ya 53, mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima na kumfanya golikipa wa Mbao kushindwa kuudaka na baada ya beki wa kimataifa wa Yanga toka nchini Togo, Vicent Bossou kuumalizia kwa kichwa na kuiandikia Yanga goli la kwanza.
Dakika ya 55, Mkongo Mbuyi Twite anarusha mpira unaomponyoka golikipa wa Mbao, Emanuel Mseja na kuingia nyavuni na kuiandikia Yanga goli la pili na Amisi Tambwe akitumia madhaifu ya mabeki hao na kuiandikia Yanga goli la tatu na la ushindi.

Mabadiliko ya Yanga yaliifanya safu ya ulinzi ya Mbao kuanza kucheza kwa umakini zaidi hasa baada ya kuingia Donald Ngoma na kutoka Obrey Chirwa, Deus Kaseke kutoka na kuingia Juma Mahadhi pamoja na Hassan Kessy na nafasi yake kuchukuliwa na Kiungo Thaban Kamosoku.

Baada ya ushindi huo, Yanga wanakwea pipa hadi Jijini Mbeya kwenda kuvaana na Mbeya City Novemba 02, na kumaliza na Prison Novemba 06  kabla ya kurejea tena Dar es salaam kuvaana na Ruvu Shooting Novemba 11.
 Hassan Kessy wa Yanga, akitafuta namna ya kuitona Ngome ya Timu ya Mbao FC, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda goli 3-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...