Mapema Septemba 2016 kwa mara ya kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Habari nchini.

Kwa sasa Muswada huu unaendelea kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Peter Serukamba na baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa ajili kuanza kujadiliwa na wabunge.

Sasa hoja yangu naielekeza katika kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu ya Tatu (c) Uthibitishwaji wa wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2) vinaelezea kuwa Mtu hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari isipokuwa kama mtu amethibitishwa na Sheria hii na (2) inasema mtu ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi wa habari ataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi utakaoainishwa katika kanuni.

Ukisoma kifungu hiki na sehemu zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo ambavyo mwandishi wa habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze kumthibitisha kuwa mwandishi wa habari kamili na baadae kumpatia Press Card.

Tukiangali kwa mifano tu ya taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka kwa Bodi zao utaona kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na kwa mfano wanasheria ili kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri wa kuwa Wakili unabidi uwe na Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya baadhi ya mitihani ya kufuzu ili kudhibitishwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...