Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara katika Mkoa wa Kigoma huku akimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu tuhuma za wizi wa madawa na ujenzi wa wodi ya kina Mama ya Buhando na ujenzi ulio fanyika Katika zahanati zingine ndani ya Manispaa ya kigoma

Hatua hiyo ya Jafo ilitokana na kutoridhishwa na utendaji wa mkuu wa idara ya Afya ya Manispaa ya Kigoma, John Maganga kutokana na usimamizi mbovu wa miradi hiyo katika idara yake sambamba na kuwepo kwa malalamiko mengi ya ubadhilifu wa madawa ndani ya Manispaa hiyo.

Jafo alitembelea jengo la wazazi la Zahanati ya Buhanda ambapo hakuridhishwa kabisa na maelezo ya ubora wa jengo hilo na mganga mkuu huyo kushindwa kumpa Naibu Waziri maelezo ya kuridhishwa juu ya gharama za ujenzi wa jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango na kuwepo mashaka makubwa ya upotevu wa fedha nyingi katika ujenzi wa jengo hilo lililo zinduliwa kinyemela na DMO huyo.

Kutokana na simtofahamu hiyo Naibu Waziri amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi ndani ya halmashauri mbalimbali hapa nchini.

Jafo katika Mikoa minne ya Mara, Simiyu, Geita na Kigoma ambapo alizifikia Halmashauri 19 na kuongea na watumishi zaidi ya 6000 pamoja na kukagua miradi mbalimbali 25 ya barabara, maji, afya, elimu na ujasiliamali imeleta tija sana kwa kuinua hamasa ya utendaji kazi kwa watumishi wa halmashauri za wilaya.

Ziara hiyo aliifanya baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Taasisi za Serikali za Mitaa (ALAT) uliofungwa rasmi tarehe 24 September 2016 mjini Musoma Mkoani Mara. Ziara ya Naibu Waziri huyo ilianza tarehe 25 September hadi 30 September 2016 ambapo alikagua miradi na kuongea na watumishi.

Jambo kubwa lililo sisitizwa Katika ziara hiyo ni umuhimu wa watumishi wa halmashauri kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma zao pamoja na kuweka maslahi ya Taifa mbele.Aliwataka wakurugenzi kuwekeana malengo ya utekelezaji na wakuu wao wa Idara, na wakuu wa idara kuwekeana malengo na watendaji wao wa chini wanao waongoza.

Kadhalika, Aliwataka watendaji wa halmashauri wabadilike katika utendaji wao. Amewataka wakuu wa idara kutowabagua baadhi ya watumishi katika idara zao.



Naibu Waziri Selemani Jafo akiwa na mtoto wa baba wa Taifa Madaraka Nyerere pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Edo Mapunda, nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Butiama.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Mbogwe Silivester Massele wakikagua jenereta la kusukuma maji Katika wilaya ya Mbogwe.


Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akikagua mradi wa Maji Katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Naibu Waziri Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara mjini Musoma
Naibu Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo akikagua kiwanda cha vijana cha kutengeneza Chaki mjini Maswa mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...