Mwanamke raia wa Brazil alietambulika kwa jina la Vera Lucia da Silva mwenye umri wa miaka 44 aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza.

Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.

Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika alhamis ya November  3 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.

Ndugu zake walipingana sana na wazo lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho.
Mmiliki wa eneo la kuzikia liitwalo Eternal Garden Funeral home, Paulo Araujo, aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote, kama mgeni maalumu.

Wakati akiwa ndani ya Jeneza mwanamke huyo alikua akifumbua macho na kufumba kama vile mtu aliyekufa na kufufuka. 

Mwanamke huyo amesema alikuwa na ndoto ya kulala kwenye Jeneza tangu miaka 14 iliyopita na hakuwa akifikiri ingekuja kutokea akaitimiza, kwasasa amefurahi kutimiza alichokitaka kabla hajafa.

UKISTAAJABU YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Astaghfirullah!
    Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utaona ya Firauni.
    Kifo hakina mazowea, ni amali zetu ndio zitakazo determine khatma zetu kwa kila mmoja wetu hiyo siku ya siku wakati 'Saqaralul Mauti' ya kila mmoja wetu itakapomfikia. Tuache kufanya mizaha itakayotupelekea kumkufuru Muumba. Kifo hakina mazowea na wala hakizoweleki kabisa! Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...