WATANZANIA takribani asilimia 40 wanatakiwa wawe wamejiingiza kwenye uchumi wa
viwanda mpaka kufikia 2020 ili kuweza kusaidia kukuza ajira za vijana na kuifanya
Tanzania kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.
Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo
ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage amesema kuwa Serikali imeazimia
kufikisha asilimia 40 ya watanzania kufanya shughuli za uchumi wa viwanda kufikia
2020.
“Tunataka mpaka kufikia 2020 watanzania takribani asilimia 40 wawe wamejikita
kwenye uchumi wa viwanda ili kusaidia kukuza ajira kwa vijana na kuifanya Tanzania
kuwa kwenye uchumi wa kati kwa maendeleo ya jamii nan chi yetu kwa ujumla”
alisema Waziri Mwijage.
Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa Uchumi wa viwanda unatakiwa kukua nchini
kuwezesha kuzalisha bidhaa bora zitakazouzwa ndani na nje ya nchi ili kukusanya
kodi kwa ajili ya kupata huduma bora za kijamii kwa maendeleo ya wananchi wa
Tanzania .
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage akiongea na wadau mbalimbali wa biashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kutumia msimbomilia(barcode) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage wa pili kulia akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kulia akimpa mkono wa pongezi Afisa Mkuu wa elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa kudhamini mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage kushoto akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Shea illushion kulia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam. Na Mpiga picha Wetu . Dar es salaam.
HABARI ZAIDI SOMA HAPA
HABARI ZAIDI SOMA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...