Picha na Habari za Freddy Macha, London 
Balozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia  jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS)  Jumamosi iliyopita. 
Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose. 
Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania”  Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa.
Wajumbe wa BTS wanaipenda Tanzania na kusimamia miradi tele kwa kujitolea bila hata senti moja. Mwaka 2015-2016 BTS imeendeleza mipango 46 ya maendeleo haya.
Mama Balozi alizungumza kifupi akisisitiza masuala muhimu ya maendeleo ya elimu, uongozi  mpya wa Rais John Magufuli unaosisitiza “Hapa Kazi Tu” katika kipindi cha mwaka mzima. Baada ya hapo alitumia muda mwingi kujibu maswali ya wajumbe. Aidha masuala yalijibiwa  au kupewa ahadi ya kufuatiliwa kivitendo. 
Wajumbe wa BTS wanaipenda Tanzania na kusimamia miradi tele kwa kujitolea bila hata senti moja. Mwaka 2015-2016 BTS imeendeleza mipango 46 ya maendeleo haya. Mama Balozi alizungumza kifupi akisisitiza masuala muhimu ya maendeleo ya elimu, uongozi mpya wa Rais John Magufuli unaosisitiza “Hapa Kazi Tu” katika kipindi cha mwaka mzima. Baada ya hapo alitumia muda mwingi kujibu maswali ya wajumbe. Aidha masuala yalijibiwa au kupewa ahadi ya kufuatiliwa kivitendo.

1-balozi-migiro-akihutubia-jumuiya-ya-watanzania-na-waingereza-pic-by-f-machaBalozi wetu Uingereza, mheshimiwa Dk Asha Rose Migiro alihutubia jumuiya ya Watanzania na Waingereza (British Tanzania Society- BTS) Jumamosi iliyopita. Hotuba hiyo iliyofanyika ukumbi wa Central Hall Westminster, London ni mara ya pili kwa balozi huyu mgeni kukutana na BTS. Mwezi Julai alikaribishwa rasmi akiwa na Balozi mpya Uingereza Tanzania Bi Sarah Cooke na aliyestaafu, Bi Diana Melrose.8-bango-la-bts-pic-by-f-macha-2016Mada hiyo iliyoitwa “Maendeleo ya Sasa Tanzania” Ilikuwa sehemu ya mkutano wa 41 wa mwaka wa BTS na kuhudhuriwa na Watanzania na Waingereza wakazi hapa.
2-petronilla-mwakaluma-akiuliza-swali-pic-by-f-macha-2016Mtanzania na mwanachama wa BTS, 
Bi. Petronilla Mwakaluma akiuliza swali3-balozi-migiro-akijadiliana-na-wataalamu-hapa-dk-gideon-mlawa-pic-by-f-machaBalozi Migiro akijadiliana na baadhi ya wataalamu Watanzania waliokuja kumsikiliza. Aliye naye “maso kwa maso” ni mganga shupavu wa kisukari Dk. Gideon Mlawa. Kulia kwake ni mwanafunzi chuo kikuu Wales, Fadhili Maghiya. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...