Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mhe. Dora Msechu amezindua harambee ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwenye Hafla iliyofanyika Stockholm, Sweden.
Hafla hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Sweden kwa lengo la kuhamasisha Watanzania waishio Sweden kuchangia wahanga wa maafa hayo. Zoezi hili maalum la uchangiaji linendelea mpaka tarehe 4 Novemba, 2016 na litahitimishwa kwa michango hiyo kukabidhiwa kwa Mhe. Balozi Dora Msechu.
Mhe. Balozi Dora Msechu akikata utepe kuzindua zoezi la uchangiaji wahanga
Mhe. Balozi Dora Msechu akiongeas kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Mji wa Malmo ambaye aliwasilisha salamu za Matanzania wa Malmo
sehemu ya washiriki wa Hafla hiyo
Mwanadiaspora Mbarouk Rashid akikabidhi mchango wa vifaa
Kocha Mkuu wa FC Kilimanjaro, Humphrey Kalanje akizungumza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...