Amiri Jeshi Mkuu Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Jumanne tarehe 29
Novemba , 2016 amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga
jijini Dar Es Salaam na kupiga marufuku
uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza
sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Rais Magufuli
amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la
Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi
kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama
kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya
hapa nchini
Hali
kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia
na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara
na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.
''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa
nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza
muda wangu , amesema Rais magufuli''
Aidha Rais
Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya
kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la
Magereza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam.
Hatua hiyo
inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani
kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi nchini na hata kuzorotesha utendaji
kazi wa askari wa Jeshi hilo.
Amiri Jeshi
Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza
kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa
ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitutumia
rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.
Rais
Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali
itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi
mengine nchini.
Jaffar
Haniu
Naibu Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es
Salaam
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja ili aongee na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016
Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza akitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...