Gari aina ya Nissan X-trial limeshika moto upande wa mbele na kuteketea gari lote. Tukio hilo limetokea jioni hii kando ya barabara ya Nyerere na usoni kabisa mwa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii, Jijini Dar es salaam. Baadhi ya wasamalia walijaribu kuokoa sehemu ya vitu vilivyokuwemo ndani ya gari hilo. Hakuna alepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hii. Chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika.
Picha na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Picha na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Moto ukiendelea kuwaka kwa kasi.
Harakati ya kuokoa baadhi ya mali ziliyokuwepo ndani ya gari hilo zikiendelea.
Baada ya muda moto ukaenea sehemu kubwa ya gari hilo, hali iliyopelekea waokoaji kushindwa kuendelea na zoezi hilo.
Moto ukiiteketeza gari hiyo.
Nissan x trail!? Dash Yaani moto Unawaka mtu Anatoa tairi
ReplyDelete