Gari aina ya Nissan X-trial  limeshika moto upande wa mbele na kuteketea gari lote. Tukio hilo limetokea jioni hii kando ya barabara ya Nyerere na usoni kabisa mwa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii, Jijini Dar es salaam. Baadhi ya wasamalia walijaribu kuokoa sehemu ya vitu vilivyokuwemo ndani ya gari hilo. Hakuna alepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hii. Chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika. 
Picha na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Moto ukiendelea kuwaka kwa kasi.
Harakati ya kuokoa baadhi ya mali ziliyokuwepo ndani ya gari hilo zikiendelea.
Baada ya muda moto ukaenea sehemu kubwa ya gari hilo, hali iliyopelekea waokoaji kushindwa kuendelea na zoezi hilo.
Moto ukiiteketeza gari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nissan x trail!? Dash Yaani moto Unawaka mtu Anatoa tairi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...