Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru leo amekutana na Balozi wa Cuba nchini Bwana Jorge Luis Lopez Tormo na kufanya  mazungumzo  yenye lengo la kuomba kupatiwa wataalamu waliobebea kwa ajili ya kutoa huduma za afya.

Katika mazungumzo hayo  pamoja na mambo mengine  Profesa Museru amemueleza Balozi wa Cuba kwamba hospitali hiyo inatoa huduma za kibingwa, lakini inakabiliwa na changamoto ya watalaam mbalimbali wakiwamo watalaam wa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU), usingizi, maabara na Radiolojia.

Amesema endapo  watapatiwa watalaamu waliobobea kutoka Cuba watasaidia kuwajengea uwezo wataalaam wa hospitali hiyo hivyo Hosptali ya Taifa itaendelea kutoa huduma bora za kibingwa.

“Hii ni Hospitali kubwa ya Taifa tunahudumia Watanzania wengi hivyo tunahitaji ushirikiano wenu kwani tukipata watalaam hao itakua hatua nzuri kwa kuwa watalaamu wetu watajifunza na kupata ujuzi na ndio maana tunahitaji wale waliobobea,”amesema Profesa Museru.

Kwa upande wake Balozi wa Cuba, Bwana Jorge Luis Lopez Tormo ameahidi kuipatia muhimbili watalaamu waliobobea ili waweze kushirikiana na watalaamu wa MHN  katika kutoa huduma sanjari na kuwawezesha madaktari na wataalamu wengine wa MNH kujifunza zaidi.

Balozi huyo pia amepata fursa ya kutembelea baadhi ya Idara ikiwamo maabara kuu, Radiolojia pamoja na Wadi namba moja ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu. 
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Jorge Luis Lopez Tormo akizungumza na wakurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) LEO katika mazungumzo ya kuimarisha huduma za afya hospitali hapo. Kulia ni ofisa wa balozi huo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo Leo.
Baadhi ya wakurugenzi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Balozi wa Cuba, Jorge Luis Lopez Tormo. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akiwa na wakurugenzi wenzake leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...