Na Dacpopo wa Globu ya jamii,

Katika harakati za Taasisi zisizo za kiserekari za kusaidia vijana kuweza kupata Elimu ili kujeng Maisha yao ya baadaye, Taasisi ijulikanayo kwa jina la Darwin imesaidia vijana wapatao 50 kupata Elimu ya vyuo vya juu nje ya nchi.

Taasisi hiyo iliyoanzishwa miezi 6 iliyopita imefanikisha kuwapatia vijana hao kupata elimu hiyo katika nchi za China,India,Malaysia,Canada na Australia.

Akieleza hayo katika hafla fupi ya kuwaaga baadhi ya vijana kwenye uwaja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo,mkurugenzi wa taasisi hiyo,Makungu Malando amesema taasisi yake inatambuliwa na T.C.U na inasaidia vijana kupata visa,malazi,usafiri na scholarship.

Naye mmoja wa wazazi ambaye mtoto wke amebahatika kupata nafasi hiyo  Hamis Suleimani,amesema kuwa anaishukuru Darwin kwa kufanikisha safari hiyo kwa kijana wake na kusisitiza kuwa taasisi hiyo inaangalia zaidi ubora wa vyuo wanavyo watafutia nafasi vijana wa kitanzania mwezi huu.
 Mkurugenzi wataasisi ya Darwin,Makungu Joseph Malando akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.
 Mzee,Hamis Suleiman ambaye ni mzazi wa mmoja wa vijana wanaokwenda kusoma katika moja ya vyuo vikuu nje ya nchi akiongea katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wataasisi ya Darwin,Makungu Joseph Malando akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na baadhi ya vijana wanaokwenda masomoni nje ya nchi katika hafla ya kuwaaga vijana wanaokwenda kujiunga na vyuo vikuu nje ya nchi kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam leo.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...