Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa 


Na Mwandishi wetu,Chunya

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa ameitaka halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha kwamba tozo zote za vijiji za Maliasili zinatozwa na zinaonekana kwenye taarifa ya mapato na matumizi.

Aidha ameitaka halmashauri kuingiza takwimu halisi za mazao yote yanayo toka katika maeneo ya vijiji husika.Agizo hilo, amelitoa leo baada ya kutembelea na kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinazoendelea katika skimu ya Ifumbo, ambayo serikali imewekeza kiasi cha shilingi milioni 900.

Amesema, licha ya serikali kuwekeza kiasi hicho cha fedha, bado eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato kwani asilimia kubwa ya mapato hayo yamekuwa hayakusanywi ipasavyo kutokana na kukithiri kwa njia za panya.

“Serikali inapoteza fedha nyingi na hii inatokana na kutokuwepo kwa mfumo bora wa ufutiliaji wa mazao hivyo mchakato huo utasaidia kuongeza mapato katika Wilaya na halmashauri yenyewe,”amesema.Hata hivyo, amesema nguvu kubwa iliyopo sasa ni kudhibiti njia zote za panya hasa katika eneo la Shoga ambalo ndio eneo linalotumiwa zaidi na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...