Na Bashir Nkoromo

Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeainisha maeneo ya magulio kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuzitaka mamlaka zinazohusika kutenga maeneo ya wafanyabiashara hao kabla ya kuwatimua katika maeneo yasiyoruhisiwa.Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Hapi, ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika kata za Kinondoni, Bunju, Msasani, Mabwepande, Kunduchi na Kata ya Wazo.

Hapi amesema, vitu vitakavyoruhiswa kuuzwa kwenye magulio hayo ni bihaa za sokoni, vyombo vya nyumbani, nguo mpya na mitumba, viatu, urembo, na kwamba kwa ujumla ni bidhaa ambazo hutumiwa na watu katika maisha ya kila siku. Ametaja mpangilo unaotakiwa kwenye magulio hayo kuwa ni, kupangwa eneo moja bidha zinazofanana, viwepo vyoo vya muda, na usafi wa eneo la gulio ambao utasimamiwa na Mtendaji Mwenyewe wa eneo husika.

MPANGILIO NA RATIBA KAMILI YA MAGULIO HAYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...