Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi.

Na Mathias Canal, Singida

Shirika la Health Actions Promotion Association (HAPA) la Mkoani Singida kwa ushirikiano na Shirika la The Foundation For Civil Society la Jijini Dar es salaam linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa vijiji vyote vya Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na mbinu shirikishi kama fursa na vikwazo katika maendeleo.

Mradi huo utaanza na Vijiji 10 vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika kata nne na kila kata itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo uchaguzi wa Vijiji hivyo vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii husika katika shughuli za maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa mradi ili kupata matokeo chanya kwa uendelezaji wa mradi husika.
 Madiwani, na Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji  Jumanne Mtaturu amesema kuwa Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na Halmashauri yataendelea katika kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea kuchukuliwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa kwa jamii kuwa na Uwezo na Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...