Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MKUU wa Wilaya Ya Kinondoni Ally Hapi amemuagiza Murugenzi wa Halmashauri Ya Wilaya ya Kinondoni Kumsimamisha kazi Mratibu wa mradi wa TASAF wa wilaya hiyo Onesmo Oyango kutokana ni ubadhilifu wa fedha za serikali kwa kuwapatia kaya ambazo hazikustahili kupewa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa maagizo hato, Hapi amesema kuwa mratibu huyo aliweza kutoa fedha taslimu kiasi cha milioni 266 kwa kaya 537 ambazo hazijulikani makazi yake na milioni 180 kwa kaya 517 ambazo hazistahili kupewa kutokana na kutokuwa na vigezo ikiwemo kuwa na uwezo wa kujikimu kimaisha na wengine ni wafanyakazi wa serikalini.

Hapi amesema, jumla ya kaya 1397 hawana sifa za kupatiwa fedha hizo za mradi wa TASAF ambazo ni mali ya serikali na zaidi inawataka TASAF kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale ambazo hawakuwa na vigezo pamoja na kuzitaka kaya hizo kurudisha fedha zote walizozichukua katila vipindi saba tofauti.

"Kama kutakuwa na njia zozote za rushwa na udanganyifu wowote katika utoaji wa fedha hizi kwa kaya ambazo hazina vigezo na zingine hazijulikani zilipo basi jeshi la usalama la Polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa zihusike mara moja kwa kuwakamata wahusika waliofanikisha ubadhilifu huo kuanzia kwa Mwenyekiti wa serikali za mitaa kwani yeye ndo wa kwanza anayewajua wakazi wake,"amesema Hapi.

Hapi amesema kuwa mbali na kaya ambazo hazikustahili kupatiwa fedha hizo, zipo zingine ambazo zinastahili ingawa hazijulikani zilipo na nyingine zimehama kutoka wilaya ya Kinondoni.

Hayo yamegundulika baada ya Mkuu huyo wa wilaya kufanya ziara katila baadhi ya maeneo na kukuta hali hiyo na tayari ametoa agizo mchakato wa kuwapatia fedha kaya zinazostahili uanze mara moja na kwa umakini mkubwa na kuvitaka vyombo vya usalama kushirikiana nao ili haki iweze kutendeka.⁠⁠⁠⁠


Mkuu wa wilaya wa Kinondoni Ally Hapi (katikati) akitoa taarifa ya ubadhilifu wa fedha katika mradi wa TASAF wilaya ya Kinondoni na kuamrisha Mratibu wa wilaya hiyo kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, kushoto ni Naibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Dennis Manumbu na kulia ni OCD wa Kituo cha Polisi Magomeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...