Na: Frank Shija, MAELEZO.

Serikali ya pongezwa kwa hatua ya kuridhia makubaliano ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, Paris 2015 UN Climate Change Conference COP21.CMP11.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhadhiri wa Heshima wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere 2016, Mhe. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akitoa muhadhara katika Tamasha la Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya Hewa leo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bilal amesema kuwa kitendo cha Tanzania kuridhia makubaliano haya ya Paris kina maana kubwa sana katika suala zima la kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia nchi na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

“Niipongeze Serikali yetu kwa kuridhia kuingia katika makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 hii itakuwa hatua muhimu sana katika jitihada za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi”. Alisema Dkt. Bilal. 

Aidha Dkt. Bilal aliongeza kuwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni makubwa sana hivyo ni vyema tukachukua tahadhari kubwa katikakuhakikisha tunakabiliana nayo.Tuweke utamaduni wa kuhifadhi na kuyatunza mazingira yetu ili vizazi vijavyo visije kupata taabu itokanayo na uharibifu wa mazingira unaoweza kuepukika.

Hakikisheni mnatunza mazingira kwani kufanya uharibifu kunapoteza uhakika wa maisha kwa viumbe hai, pamoja na kupoteza vyanzo vya mapato,hivyo ni vyema tukajiepusha na matumizi ya baruti, uvuvi haramu, ukataji miti na mikoko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...