Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji wa kampuni ya Fichtner ya Ujerumani na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kufanya ziara katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini kinachojengwa kupitia Mradi wa TEDAP ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Kampuni ya Fichtner ya Ujerumani, Matthias Albers (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Katikati ni Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere.
Mafundi wakiendelea na ujenzi katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini, kinachojengwa chini ya Mradi wa TEDAP.
Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere (kulia) akitoa maelezo kwenye kituo cha kuendesha mitambo (control room) katika Kituo Kipya cha Kupooza Umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi (Miradi) kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gregory Chegere (katikati) akisisitiza jambo katika sehemu ya kupokelea laini za umeme.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ZAIDI
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...