Na Teresia
Mhagama.
Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amezindua mradi wa umeme wa Kilowati
430 unaotokana na maporomoko ya maji katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe ambapo
mpaka sasa zaidi ya wateja 1140 wameunganishiwa umeme huku zoezi hilo likiwa ni
endelevu.
Uzinduzi huo
uliofanyika katika Kata hiyo ulihudhuriwa na Balozi wa Italia nchini
Tanzania, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa
wilaya ya Njombe, wananchi wa Kata ya Ikondo, Shirika lililotekeleza mradi huo
la CEFA, watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).
Dkt. Kalemani
alisema kuwa mradi huo umetekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya
CEFA kutoka Italia na kugharamiwa kwa pamoja kati
ya Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya Dola za Marekani
110,209.
Aliongeza kuwa
mradi huo wa umeme utasambazwa katika vijiji vilivyoko kata za Ikondo, Matembwe
na Lupembe na ziada itakayobaki inaingizwa kwenye gridi ya Taifa.
" Habari
njema ni kuwa tayari vijiji Saba vimeunganishiwa umeme kupitia mradi huu, hii
inatimiza moja ya malengo ya Serikali ya kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji
wa nishati bora katika maeneo ya vijijini kupitia asasi za kiraia,"
alisema Dkt. Kalemani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Lupembe, Joram Hongoli (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Jane Nunes (wa Tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gideon Kaunda (wa pili kulia) na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni (wa Nne kulia).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) akipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Lupembe, Joram Hongoli (wa Tatu kushoto), Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Jane Nunes (wa Nne kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gideon Kaunda (wa pili kushoto).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akiangalia moja ya mitambo ya kuzalisha umeme Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema na wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...