Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamedi Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la kibiashara la Tanzania Comoro (Trade Forum) lenye lengo la kuboresha fursa za kiuchumi baina ya nchi za Tanzania na Comoro.

Kongamano hilo ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 150 wanatakao shiriki katika kongamano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Kongamano hilo kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA, Anna Msonsa amesema kuwa lengo ni kupata kampuni zaidi ya 50 kutoka sekta binafisi kushiriki katika kongamano hilo.Mratibu huyo amesema kuwa wafanyabiashara hao watajadili mahusiano ya kibiashara, mazingira na kuweza kupata masoko kwa njia ya mahusiano mema watakayokuwa nayo.

Amesema kongamano hilo limeratibiwa na Kampuni ya 361 na kwamba litafanyika Novemba 19, mwaka huu katika Hotel ya Cliff iliyopoZanziabar. 
“Kongamano hilo litaweza kuangalia fursa za nchizi hizi mbili za Comoro na Tanzania na kuona ni jinsi gani litawawezesha kukuza uchumi,”amesema.

Naye Ofisa balozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro Mudrick Soragha 
amesema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro Said Bakara pamoja na wajumbe wengine sita.

“Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro ataongozana na wajumbe wake sita hivyo ada ya ushiriki mwaka huu tumepunguza hadi kufikia asilimia 80 kutoka asilimia 100,”amesema Soragha.Kwa upande wa Ofisa miradi wa Kampuni ya 361 Naomi Godwin aliwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi ili kushiriki kongamano hilo.

“wafanyabiashara wanaweza kupata fomu ya ushiriki kupitia mtandano wa kampuni ya 361 ili kuzijana na kuweza kupata nafasi ya kushiriki kongamano hili,”amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...