Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Young Africans hali kadhalika Mchezaji Hassan Hamisi Ramadhani maarufu kama Hassan Kessy, Wakili Msomi, Mzee Said El-Maamry anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa mwadai hayo.

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliagiza pande za Simba na Young Africans kumaliza suala hilo mapema mwezi uliopita, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake walishindwa kufanya hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka huu.

Hata hivyo, msuluhishi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka Young Africans kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa safarini Iringa alikokwenda kwa sababu ya matatizo ya kifamilia. Ilielezwa kuwa Mgongolwa ambaye ni Mwanasheria wa Young Africans, alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine.

Kutokana na hali hiyo, E-Maamry amepanga sasa kukutana nna viongozi na/ au Wawakilishi wa pande zote mbili Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia namna ya kumaliza madai ya Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni dhidi ya Young Africans ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.

Mzee El-Maamry amesema: “Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikiliszwa. Ni vema Mwanasheria wa Young Africans akasubiriwa.”

Kamati ya TFF inasuburi makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye Kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...