Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema mzunguko wa fedha sio mzuri kutokana na fedha nyingi  kwenda katika  miradi ya  kuimarisha huduma kwa wananchi.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, Msajili wa Hazina, Lawlance Mafuru wakati akizungumza na waandishi habari juu ya taarifa zinazosambaa  zinazodai kuwa benki zimeyumba.

Amesema serikali katika kudhibiti fedha za umma katika mashirika na taasisi ni kuwa na akaunti benki kuu ili kuweza fedha hizo kuonekana na sio kuwa katika benki zingine.

Mafuru amesema kuyumba kwa taasisi za fedha  haitokani na kuondolewa kwa kiasi cha sh.bilioni 515 kwa kila taasisi kuwa na akaunti benki kuu.
Amesema taasisi za fedha kwa septemba zimekopesha sh.trioni 16 kati ya fedha hizo sh.trioni 1.4 ni mikopo mibovu hivyo kwa benki lazima ziyumbe kwa muda kutokana na mikopo hiyo mibovu.

Mafuru amesema kupanga ni kuchagua hivyo serikali imetaka kuimarisha huduma kwa wananchi , lazima kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika huduma za kijamii.Amesema viwanda vikijengwa hapa  nchini wananchi watanunua bidhaa za ndani hivyo fedha itazunguka hapa hapa kuliko kununua bidhaa za nje ambazo fedha zinakwenda kuwapa maendeleo  nchi nyingine.
  
Aidha amesema kuwa nia Rais Dk. John Pombe Magufuli ni njema ya kutaka kuimarisha huduma kwa wananchi katika miradi mbalimbali zinazokusanywa.
Msajili wa Hazina, Lawlance Mafuru akizungumza na waandishi wa habari juu hali ya mzunguko wa fedha leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...