Na Hamza Temba - WMU
Kufuatia malalamiko ya wahifadhi juu
ya kauli na vitendo mbalimbali za baadhi ya wananchi na viongozi wa kisiasa vyenye
lengo la kukwamisha shughuli za uhifadhi nchini kwa maslahi yao binafsi kwa
visingizio kuwa ni maagizo kutoka juu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa
tamko na kusema kuwa hakuna kiongozi wa juu wa Serikali anayepinga zoezi la uhifadhi
wa maliasili nchini.
Majaliwa
ameyasema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi na watendaji wakuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, wakuu wa taasisi za uhifadhi zilizopo chini ya wizara
hiyo na wakuu wa hifadhi za taifa pamoja na mapori ya akiba katika kikao
alichokiitisha kwenye ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.
“Wapo watu
wanaotumia majina ya viongozi wakuu kukwamisha mazoezi yanayoendeshwa na
wahifadhi nchini. Hakuna kiongozi wa juu anaeweza kuzuia zoezi muhimu kama
hili. Na Kama kuna mtu anakuja kukuambia wewe fulani kasema, mwambie
niunganishe na yeye mwenyewe. Tumeona maeneo mengi sana, watu wanafanya
madudu wanasema huyu kaagizwa kutoka juu, juu ni wapi, kwa Mkurugenzi wako? kwa
Katibu Mkuu? Naibu Waziri au Waziri? Au huku kwa Waziri mkuu? Makamu wa
Rais au Rais?,” alihoji.
“Fanyeni,
bora ukosee halafu tuseme hapo umekosea utarekebisha, kuliko kuogopa kufanya
kwa sababu mtu kakukwamisha, kwani ulivokuwa unaimplement (unafanya) alikuambia
nani? si kutokana na na sheria na taratibu, muhimu zaidi ni kuzingatia sheria
na taratibu, usije ukafanya mambo ya ajabu,” aliongeza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...