Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiizi wa Mazingira Nchini, NEMC limeipiga faini ya shilingi milioni kum na tano Halmashauri ya wilaya ya Kahama kwa kile kinachodaiwa ni uzembe wa kuto zingatia sheria ya mazingira kwa kuliweka Dampo la mji huo katika hali hatashi kwa mazingira na viumbe hai wengine.
Katika Ziara ya Naibu Waziri Mpina Leo Mjini Kahama, ilohusisha ukaguzi wa Dampo, machinjio viwanda na soko la mjini kahama kumebainika kuwa na uzembe kwa watendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wa kutosimamia utupwaji wa taka katika Dampo la mji huo ulohusisha kutupwa kiholela kwa taka ardhini na kuteketezwa kwa njia isiyo salama.
Kufuatia ukiukwaji wa sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake, Baraza la mazingira nchini  NEMC limeshawishika kuitoza faini Halmashauri hiyo ya shilingi milioni kumi na tano na kutakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili.
Akiitaja adhabu hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mkaguzi wa NEMC kanda ya ziwa na Mikoa jirani Bw. Jamali Baruti sambamba na hilo ameleza kuwa, Halmashauri ya Kahama inatakiwa kuboresha miondombi ya taka,kuratibu na kusimamia ujenzi wa mabwawa katika machinjio mjini hapo kwani utupwaji holela wa samadi huchangia uharibifu wa mazingira.
Akitilia msisitizo wa suala zima la uzingatiaji wa sheria ya mazingira kwa watendaji nchini, Naibu Waziri Mpina alisema kuwa hawezi kukubali kuwajibishwa sababu ya viongozi kushindwa kusimamia suala zima la mazingira, na kuhaidi kuwawajibisha viongozi wazembe.
Awali, akitoa taarifa ta usafi wa mazingira ya wilaya ya Kahama Mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Nkulu alisema kuwa Kahama imekuwa ikikabiliwa na chngamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni Pamoja na uhaba wa magari ya kuzolea taka, ukataji miti kwa matumizi ya kukaushia tumbaku, na usafishaji wa dhahabu kwa kutumia madini ya zebaki ambayo si rafiki kwa mazingira.
Ziara ya Naibu Waziri  Mpina wilayani Kahama ni Muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkulu akitoa taarifa ya usafi wa mazingira ya Wilaya Hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muunano na Maingira Mhe. Luhaga Mpina na Ujumbe wake hawapo pichani, katika siku ya kwanza ya ziara ya Naibu Waziri Mpina  ya ukaguzi wa mazingira Wilayani Kahama.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina mwenye T-Shirt ya mistari mnyeupe, na baadhi ya ujumbe wake katika ziara Mjini Kahama wakiangalia sehemu ya uzalishaji wa bati katika kiwanda cha Kahama Oil Mills ltd, kinavyokunjwa na kutoka katika mashine, ikiwa ni siku a kwanza ya Ziara ya Naibu Waziri Mpina leo. 
 Kati kati mwenye t-shirt ya mistari mnyeupe, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na sehemu ya ujumbe wake katika ziara ya ukaguzi wa DAMPO la Busoka Wilayani Kahama Leo.
 Sehemu ya taka ngumu zilizotupwa kiholela katika kiwanda cha kutengeneza mafuta yatokanayo na pamba cha  Kahama Oil Mills Ltd, cha Mjini Kahama chenye kukabiliwa na changamoto ya utengaji, utunzaji na utupaji taka ngumu kiholela kiwandani humo ambapo Naibu Waziri Mpina alikitembelea Leo. (Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...