Halmashauri  ya wilaya  ya Namtumbo  mkoani  Ruvuma   hivi  karibuni  imeanza  mchakato  wa kuanzisha  Redio  ya  jamii (community  radio )itakayorusha  matangazo  yake  ndani  ya wilaya  hiyo   ya  Namtumbo.

Ofisa  habari  wa  wilaya  ya  Namtumbo  Yeremias  Ngerangera  alisema  kuwa  mchakato  wa  kuanzisha  Redio  hiyo  ya  jamii unaendelea  vizuri  ambapo  kwa  hatua  ya awali  kamati  ya kuanzisha  Redio  iliundwa  na tayari  kamati  hiyo  imeanza kazi yake .

Bwana  Ngerangera  alitaja  idara  zilizopo kwenye  kamati  hiyo  ni  idara  ya  mipango,idara  ya  utawala,idara  ya maendeleo  ya  jamii, idara  ya  afya ,idara  ya mazingira  pamoja na kukihusisha  kitengo cha  sheria  na usalama .
Aidha  bwana  Ngerangera  alibainisha  sababu  za  halmashauri  hiyo  kuanzisha  Redio hiyo  ni  pamoja na  kurahisisha mawasiliano  kati  ya  uongozi  wa  halmashauri  hiyo  na wananchi  wake juu ya  maagizo  mbalimbali  ambayo  halmashauri inawataka  wananchi  wake kufanya.

Pia  redio  hiyo   itatumika pia kuelimisha  jamii ya  Namtumbo kuhusiana  na  kilimo bora ,umuhimu  wa utunzaji  wa  mazingira ,umuhimu  wa kuwapatia  watoto  elimu,umuhimu  wa kuwa na afya bora pamoja na  kuwatangazia  wananchi mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

Kaimu  afisa  mipango  wa Halmashauri  ya  wilaya  ya  Namtumbo  Gwakisa  Mwaseba  ambaye  pia  ni  mwenyekiti  wa  kamati  ya kuanzisha  Redio  hiyo  alisema  kuwa  zaidi  ya milioni 103,400,000 zinahitajika  ili kukamilisha  zoezi  la kuanzisha redio hiyo.

Bwana  Gwakisa  aliwataka  wadau  kutoka  sehemu mbalimbali  katika  nchi  hii ,wazaliwa  wa wilaya  ya  Namtumbo  na wenye  mapenzi  mema  na  Halmashauri  ya wilaya  ya Namtumbo  kushirikiana katika kuhakikisha  redio  hiyo  inaanzishwa .
Pamoja  na mambo  mengine  aliwaomba  wadau  kuchangia uanzishaji  wa  redio  hiyo kwa kuwa redio  hiyo itakuwa  na umuhimu mkubwa kwa  Halmashauri  yetu ya Namtumbo  na wilaya nzima ya Namtumbo.

Mkurugenzi  wa  Halmashauri  ya Wilaya ya Namtumbo  Christopher  Kilungu  aliitaka kamati  hiyo ya kuanzisha Redio  kufanya  mikutano yao na kuwasilisha mapendekezo ya kamati  yao  kwenye uongozi  wa Halmashauri kwa lengo  la kujiridhisha  na kuyajadili mapendekezo  hayo .

Pamoja  na mambo  mengine  mkurugenzi  huyo  aliitaka  kamati  hiyo kufanya  kazi  yake  vizuri  na  kuhakikisha  Redio  hiyo  ya  Halmashauri  inaanzishwa  kwa madai kuwa Redio  hiyo  itakuwa  na tija kwa maendeleo  ya wananchi  wa Namtumbo  na Halmashauri  yao.

Wananchi  wa wilaya  ya Namtumbo  walipoelezwa  kupitia  mikutano  ya Hadhara  kuhusiana  na Hatua  ya kuanzisha Redio  hiyo  walifurahishwa  na hatua hiyo kwa madai ya kuwasaidia katika kutoa  maoni  yao kupitia kadi za salamu zitakazosomwa  kwenye Radio  hiyo.

Halmashauri  ya  wilaya  ya  Namtumbo  ina jumla  ya Tarafa  Tatu, kata  ishirini  na  moja  na vijiji  sabini  na moja  ambapo ina ukubwa wa kilomita  za mraba 20,375.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...