Hospitali ya kairuki katika kuboresha huduma zake kwa wagonjwa imeanza kutumia kitengo kipya kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kutwa hususani wale wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kitengo hicho kipya (OPD 3) kilichopo nyuma ya Jengo kuu la hospital mkabala na kitengo cha magonjwa ya viungo ( Physiotherapy Unit).
 

 kina sehemu kubwa ya mapokezi, vyumba mbalimbali vikiwemo vyumba 10 via madaktari, maabara,Duma la dawa,sehemu ya sindano na kufunga vidonda,chumba cha ultrasound,mapokezi , huduma za chanjo ya watoto (RCH),chumba cha wauguzi na duka dogo la vinywaji na vitafunwa nk .
Kitengo hicho kipya kitaiwezesha hospital hiyo kutoa huduma kwa haraka na ufanisi kwa wagonjwa wasiopungua 120000 kwa mwaka hivyo kupunguza Kero ya foleni na msongamano iliokuwepo siku za nyuma.
Aidha kitengo hicho (OPD3) kitazinduliwa rasmi hivi karibuni pamoja na vitengo vipya vya kusafishia figo ( Dialysis Unit) na kile cha huduma za dharula ( Emergency Unit)
Pichani ni Majengo mapya ya kisasa yatakayokuwa yakitumika kutoa huduma.
Pichani wagonjwa wakisubiri kupata huduma Muda mfupi Mara baada ya majengo hayo kufunguliwa.
Pichani wagonjwa wakisubiri kupata huduma Muda mfupi Mara baada ya majengo hayo kufunguliwa. Na Afisa Mahusiano;Arafa Mohamed

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...