Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa mashine kubwa na ya kisasa ya Utra Sound maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya Figo. Msaada huo umetolewa na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba. 
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal Ruggajo amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua magonjwa ya Figo, kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo. 
“ Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali hiyo , MUHAS na MNH na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo , wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” amesema Dk. Ruggajo. 
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk . Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru Hospitali hiyo ya Haukeland na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwakua mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha Figo.
 :   Profesa Einar Svastard ( kulia)   akimkabidhi  msaada wa mashine kubwa ya kisasa ya Utrasound  Mkurugenzi wa huduma za tiba  MNH Dk. Hedwiga Swai  .
 Dk. Hedwiga Swai ( kushoto ) akimshukuru Profesa  Svastard kwa msaada walioutoa kwa niaba ya Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru.
 Hii ndio mashine  ya  Utrasound ambayo itatumika kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua magonjwa  ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo.
Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...