Inaitwa Lulu kwa lugha ya Kiswahili. Kwa lugha ya Kiingereza ni Pearl. Hicho ni kito cha thamani ambacho mara nyingi kinakatwa, kusuguliwa na kung'arishwa kwa namna mbalimbali na kutumiwa pamoja na madini mengine kama dhahabu au fedha na kutengenezwa mapambo kama pete, hereni, mikufu au vikuku.

Lulu inatajwa siku nyingi kuanzia katika misahafu ambavyo ni vitabu vitakatifu kwa waumini wa dini ya Kiislamu hadi katika Bibilia na hadithi nyingine za kale. Nchini kuna utajiri mkubwa wa Lulu, lakini hakuna jitihada zozote za kuvuna kito hicho cha thamani ambacho moja ya sifa yake kuu ni kutobadilika rangi yake kwa namna yoyote katika kipindi chote cha kudumu kwake labda iharibiwe kwa tindikali.
Lulu ni nini?

Kito hicho ni tofauti na madini ya almasi, dhahabu, Tanzanite, Ruby na madini mengine ambayo yanachimbwa, lakini Lulu inatokana na wanyama (katika viumbe hai aina ya chaza/Oyster) jambo ambalo huenda watu wengi hawalifahamu.

CHAZA NI VIUMBE WA PEKEE SANA DUNIANI KWANI HUZALIWA WOTE WAKIWA MADUME NA KUBADILIKA KUWA MAJIKE MIAKA MITATU BAADA YA KUWAPO DUNIANI NA WANAWEZA KUJIGEUZA TENA KUWA MADUME BAADA YA KUTOTOA MAYAI......
(All pearl oysters are born male and transform into females at around three years of age. Even more remarkably, after releasing her eggs, the female oyster may turn male again! This change can happen in under a month!)

Lulu ni moja kati ya mazao ya bahari ambayo kama yangetumika vizuri yangewanufaisha wakazi wa Pwani na Taifa kwa ujumla kuliko sasa. Kwa kawaida chaza ana magamba na chakula chake hukipata baada ya kuyachuja maji ambayo mintaarafu anayavuta baada ya kufungua na kufunga magamba yake na wakati wa tendo hilo kuna mabaki ambayo ni chakula kwake hubakia.

Nyama yake inahusishwa na kuongeza virutubisho mwilini na kuchochea ongezeko la homoni ambazo zinaongeza nguvu za kiume kwa wanaume na upande mwingine gamba la mnyama huyo hutumika kama mapambo majumbani na kwingineko.

​Geofrey Chambua Kutoka Vyanzo Mbalimbali ​

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Je lulu ina ukubwa au uzito gani? na vipi bei yake?

    ReplyDelete
  2. Kwa hapa Dar-es-salaam au mikoani Ni sehemu gani wananunua Lulu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...