Mhadhama Kardinali Polycarp Pengo na Dkt.
Fredrick Kigady wakifuatilia historia fupi ya Tuzo ya BENEMERENTI ambayo upewa
mtu aliyetoa mchango wake mkubwa katika kutumikia jamii pamoja na kanisa wakati
wa hafla ya kumkabidhi tuzo hiyo Dkt. Kigadya mapema wikiendi hii Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
(TEC) Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akizungumza katika hafla fupi ya
kumkabidhi tuzo na kumvisha nishani Dkt. Fredrick Kigadye aliyotunukiwa na Baba
Mtakatifu Papa. Francis mapema wikiendi
hii. Kushoto ni Mhadhama Kardina Polycarp Pengo, Dkt Fredrick Kigadye na Mkewe.
Muadhama Kardinali Polycarp Pengo akimkabidhi
hati yenye ujumbe maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu Papa. Francis Dkt. Fredrick
Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo aliyetunukiwa kufuatia mchango wake
mkubwa katika kulitumikia Kanisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza
la Maaskofu Tanzania (TEC) mapema wikiendi hii. Kulia ni Mke wa Dkt. Kigadye
akishuhudia tukio hilo.
Muadhama Kardinali Polycarp Pengo akimvisha
nishani ya heshima ijulikanyao kwa jina la Benemerenti
(Anayestahili) Dkt. Fredrick Kigadye aliyetunukiwa tuzo hiyo na Baba Mtakatifu
Papa Francisco kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Katisa Katoliki kupitia
Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) jana Jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Mke wa Dkt. Kagadye akishuhudia tukio hilo.
Dkt. Fredrick Kigadye akitoa neno la shukrani
kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kutambua mchango wake katika
jamii na kanisa kwa ujumla. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...