Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga akisalimiana na Baadhi ya
Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dar es Salaam alipofanya ziara ya
kukagua maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi
hilo leo Novemba 30, 2016.
Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir
Minja(katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius
Mwakalinga wakiangalia moja ya eneo la Gereza Segerea ambalo litajengwa nyumba
za kuishi za Maafisa na askari wa Jeshi hilo(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kuu
Segerea, ACP. Godfrey Kavishe
akiwaonesha eneo hilo walipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya Jeshi
ambapo tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba
za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Moja ya eneo litakalojengwa nyumba za Maafisa na
Askari wa Jeshi la Magereza lililopo katika eneo la Gereza Kuu Segerea, Jijini
Dar es Salaam kama linavyoonekana katika picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana
na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu pamoja
na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo waliopo katika Magereza ya Mkoa wa Dar es
Salaam wakitembelea maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za
watumishi wa Jeshi hilo.
Moja
ya nyumba ya mabati iliyopo katika Gereza la Mahabusu Keko kama inavyoonekana katika
picha. Katika kukabiliana na uhaba wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza
Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
(Picha
zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Rais JPM aonyesha urais shupavu na shujaa.
ReplyDeleteRais JPM afanya majeshi yawe sawa kwani yote huenda vitani.
Lakini rais JPM uwakumbuke nao kwenye kamisheni.
Pia rais JPM uwakumbuke kwenye mishahara.
Unification katika kozi ya awali. Gharama lakini imara, hakuna cha bure, dezo inaua.
Ombi: kozi ya recruit ya kuwa private iwe kwa majeshi yoote bila kujali. hii itaongeza uwezo wa kushinda vita. Vita ya uganda ilitumia muda mrefu na vifo vya wapiganaji vilikuwa vingi kwa sababu askari wa majeshi yasiyo JW hawakuwa fiti saana kwa sababu ya kutofautisha mafunzo ya awali wakati wakati JW wenyewe wachache hawahkutosha. Risasi hauchagui askari lakini askari mwenye mafunzo sahihi atalenta ushindi na kuepuka vifo na majeruhi wasiyo lazima. Azma yako uliyosema nimekusapoti.