Wakati msimu mpya wa kilimo ukiwa unatarajiwa kuanza, Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) imeanza zoezi la kusambaza mbolea ya ruzuku kwenda katika mikoa inayotarajia kuanza msimu wa kilimo wa 2016/2017.
Akiongea na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania, Bwana Salum Mkumba amewataka wakulima kujiandaa kupokea mbolea ya ruzuku ambayo imeanza kusafirisha tangu jana tarehe 7/11/2016 kutoka kwenye maghala ya Kampuni hiyo yaliyopo Jijini Dar es Salaam kwenda Mikoa 20 ya Tanzania Bara.
Bwana Mkumba amesema kuwa kwa zoezi la kusambaza mbolea hiyo ya ruzuku, litahusisha kiasi cha tani 32,300 (Tani elfu thelasini na mbili na mia tatu) ambazo zinaigharimu Serikali fedha kiasi cha shilingi bilioni 12 ambapo mkulima atapaswa kununua mfuko wa mbolea ya kupandia au kukuzia wa kilo 50 kwa shilingi 30,000.
Bwana Mkumba aliongeza kuwa mbolea hiyo imeanza kupelekwa katika Mkoa wa Katavi na Mikoa minginge ya Nyanda za Juu Kusini, Mikoa hiyo matumizi ya mbolea yapo juu na kwamba zaoezi hilo litaendelea kwenda Mikoa mingine kwa kutumia usafiri wa Reli na Barabara mpaka kukamilisha zaidi ya tani 32,000 zilizokusudiwa.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Pembejeo, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Bwana Shanil Nyoni amesema, lengo la Serikali ni kuiwezesha Mikoa 20 kupata mbolea hiyo na ndivyo itakavyokuwa na kwamba Mkoa wa Katavi na Rukwa inaanza kupata mbolea hiyo kwa sababu, msimu wa kilimo unaanza hivyo itawafikia kwa wakati.
Bwana Shanil ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuwasaidia wakulima wasio na uwezo wa kumudu kununua mbolea na kwa utaratibu unaanza kwa kuwatambua wakulima kuanzia katika  ngazi ya Kijiji wenye sifa ya ukaazi wa eneo hilo, mwenye eneo la kulimia mahindi kuanzia ekari moja, na awe mkulima aliyetayari kupokea utaalam wa matumizi ya pembejeo hizo, ikiwemo mbolea na mbegu bora na awe tayari kuchangia gharama kidogo na kuongeza kuwa kwa kuanzia mpango huu umelenga kuwafikia wakulima laki tatu.
Aidha Bwana Nyoni amewataka wakulima kuondoa hofu ya kuwa mbolea hizo zinadumaza mazao na badala yake zinaongeza tija na uzalishaji kwa kuwa zimefanyiwa utafiti kabla ya kuwafikia wakulima kulingana na udongo na aina ya mazao.  
 Mkurungezi Msaidizi wa Pembejeo za Kilimo Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvvi Bwana Shanil Nyoni akizungumza na Waandishi wa Habari 
 Meneja Mkuu wa Kampuni  ya Mbolea Tanzania Bwana Salum Mkumba akisema jambo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mbolea  Tanzania (TFC) wakipakia mifuko ya mbolea ya ruzuku tayari kwa kusafirishwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...