Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni  ya Start My Safari, Joshua Sewe (Kushoto) akifanunua matumizi ya kifaa maalum kitumikacho katika ukataji wa tiketi za mabasi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Doris Kini Afisa Huduma kwa Wateja na Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo Bw. George Mlambala(Kulia).
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Start My Safari, Bw. George Mlambala (Katikati) akifanunua matumizi ya kifaa maalum kitumikacho katika ukataji wa tiketi za mabasi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Doris Kini Afisa Huduma kwa Wateja na Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo Bw. Joshua Sewe (Kushoto).


Kampuni ya Start My Safari Limited imeziwezesha kampuni 25 za mabasi hapa nchini kuanza kutumia teknolojia mpya ya ukataji wa tiketi kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti kuwakatia tiketi wateja wao.

Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Start My Safari iliyoingia makubaliano na wasafirishaji hao, Geoorge Mrambala amesema kuwa, kwa sasa watanzania wanaweza  kukata tiketi mahali popote na wakati wowote kwa kutumia mifumo hiyo ya mawasiliano.

“Hakuna gharama za ziada katika ukataji wa tiketi, yaani abiria analipa nauli ileile iliyoidhinishwa na serikali na ndani ya dakika chache anatumiwa tiketi yake ya kielektroniki,” amesema.

Amesema mfumo huo pia unawafuatilia wateja wao kuanzia wanapokata tiketi, kabla ya safari, wawapo safarini na wanapoahirisha safari.
Meneja huyo amesema mfumo unamrahisishia msafiri kujua basi atakalosafiri nalo kama anavyotaka mwenyewe, muda atakaofika na awapo njiani anafuatiliwa mpaka anapofika aendako.

“Huduma hii kwa sasa inapatikana kirahisi zaidi kwa watumiaji wa smartphone, lakini pia hata kama hana simu hiyo anaweza kutuma ujumbe mfupi na moja moja anatumia tiketi na kuunganishwa na basi atakosafiri nalo na inapatikana pia kwa njia ya mtandao,” alisema.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...