NA ANTHONY ISHENGOMA.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga leo amefungua  mkutano wa mashauriano wa kanda ya Afrika kuhusu Mtandao wa Kuzia Unyonyaji  na Usafirishaji  wa Watoto kwa lengo la kuwafanyisha ngono.

 Akiongea katika Mkutano huo Bi Sihaba Nkinga amesema Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika imeridhia na kutekeleza mikataba mbalimbali ikiwemo kutunga sera na sheria pamoja na  mikakati ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto.

Aliendelea kusema mwaka huu Tanzania ni Nchi pekee barani Afrika ambayo imechaguliwa kama nchi ya kuigwa kwenye juhudi za dunia kupambana ukatili wa wanawake na watoto akizataja Nchi nyingine kuwa za Mexico, Indonesia na Sweden.

Katibu Mkuu Sihaba Nkinga amesema kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya Nchi zinazounda ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ukatili wa Wanawake na Watoto kwasababu ilikuwa Nchi ya pili duniani kuitikia wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa kufanya tafiti za ukatili dhidi ya  Wanawake na Watoto barani Afrika. 

Akiongea katika Mkutano huo wa mtandao wa kuzuia unyonyaji kingono kwa watoto Afrika Bi. Sihaba Nkinga amesema  taarifa ya utafiti huo ilyofanyika mwaka 2009 na kusambazwa mwaka 2011 ilitoa majibu ya yaliyonesha kuwepo kwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika ngazi zote ikiwemo ngazi ya familia, shule na njiani kuelekea shuleni.

Aidha ameviambia vyombo vya Habari vilivyokuwepo katika Mkutano huo kuwa hii ndio sababu kwasasa Tanzania inajipanga kuzindua Mpango Mkakati wa kupambana na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto mapema tarehe 13 mwezi desemba.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la KIWOEDE Bi. Justa Mwaitaka amesema mtandao huu unakutana kujadili namna bora ya kupeana taarifa za Watoto wanaosafirishwa kwa lengo la kunyonywa kingono ndio maana kuna Nchi 21 kutoka barani Afrika.

Aliongeza kuwa Mkutano huu utaangalia sheria zilizopo kama zinakidhi haja ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto akizitaja sheria za Tanzania kuwa na utaratibu unaochelewesha upatikanaji wa haki za watoto pindi inagundulika kuwepo kwa ukatili dhidi ya watoto taratibu za kisheria na kimahakama zinakuwa ngumu katika utekelezajia wake.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akifafanua jambo kwa vyombo vya habari kuhusu Mkutano wa Mtandao wa Kimataifa wa kuzuia unyonyaji na usafirishaji wa watoto kwa lengo la kuwafanyisha ngono unaoendelea leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga pamoja na baadhi ya Wajumbe wa bodi ya Mtandao wa Kupambana na Usafirishaji na unyonyaji watoto Kingono Duniani wakifuatilia maendeleo ya Mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Kupambana na Usafirishaji na unyonyaji watoto Kingono leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...