Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

Wadau mbalimbali wa Mashirika ya Kiraia na Sekta binafsi kwa kushirikiana na TUME ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wanatarajia kukabidhi ripoti maalum kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi ifikapo Desemba mwaka huu ripoti hiyo ikiwa ni ya uandaaji wa mpango kazi wa utekelezaji wa Makubaliano ya Mkutano mkuu wa Wadau wa Mipango ya Matumizi ya ardhi nchini .

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kikosi kazi uliofanyika mkoani Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Dk Stephen Nindi alisema vitu muhimu katika nchi ambavyo vinasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ni upangaji wa matumizi bora ya ardhi.

Alitaja vitu ambayo ni miongoni vinavyokwamisha kwenda kwa kasi kwa zoezi la upangaji wa matumizi bora ya ardhi ni pamoja na ufinyu wa bajeti na ukosefu wa teknolojia mpya zinazoweza kupima na kupanga ardhi kwa mwendo wa haraka zaidi.
 Kikosi kazi katika mkutano wa siku mbili uliofanyika Morogoro
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania Dr. Stephen Nindi akichangia jambo wakati wa mkutano huo
 Bw.Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...