Na Theresia Mwami TEMESA

Kivuko cha Magogoni kinakusanya hadi jumla ya shilingi milioni 17 kwa siku za kazi kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kutokana na kutoa huduma ya kusafirisha abiria, mizigo na magari kwa kutumia vivuko vya MV Magogoni na MV Kigamboni.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni Mhandisi Lukombe King’ombe alipokuwa akitoa taarifa ya kivuko hicho kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu alipotembelea kivuko hicho hivi karibuni.

Mhandisi King’ombe aliongeza kuwa kwa sasa wanakusanya mpaka milioni 17 kwa siku za Juma na kwa siku za mwisho wa wiki yaani Jumamosi na Jumapili kiasi hupungua kidogo kutokana na abiria wengi kutotumia kivuko hicho.

 Aidha Mkuu wa Kivuko cha Magogoni Mhandisi Kin’gombe alimueleza Dkt. Mgwatu kuwa hali ya makusanyo hivi sasa inaridhisha kwani abiria wengi wameanza kurudi kutumia kivuko hicho baada ya kujiridhisha kuwa  MV Magogoni imerudi kutoka kwenye ukarabati mkubwa na sasa inafanya kazi vizuri. 

Kwa upande wake Dkt. Mgwatu alimuagiza Mhandisi King’ombe kuhakikisha kuwa wanaziba mianya yote ya upotevu wa mapato kivukoni hapo ili kuhakikisha wanafikia lengo la kukusanya shilingi milioni 19 kwa siku ambayo ni agizo la Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa alipotembelea kivukoni hapo mapema mwezi Oktoba mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi TEMESA alitembelea na kukagua kivuko cha Magogoni ili kujiridhisha utendaji kazi wa kivuko hicho.
Mhandisi Lukombe King’ombe (kulia) akifafanua jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) alip tembelea chumba cha mifumo ya kuendeshea Kivuko cha MV. Magogoni.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dk. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) akikagua taarifa za mitambo ya kuongozea Kivuko cha MV Magogoni.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dk. Mussa Mgwatu (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko Cha Magogoni Mhandisi Kingo’ombe Lukombe (Kulia), alipotembelea kivuko hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wabongo kwa uharibifu bwana, nina uhakika waliotengeneza kivuko walikuwa hawatumii madumu ya OKI.

    angalia hata storage ya hayo madumu, kienyeji enyeji sana. hakuna health and safety hapo mpaka litokee janga....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...